The House of Favourite Newspapers

Watoka Zanzibar Kwa Vespa Kwenda Dodoma Kumpelekea Rais Dk. Samia, Maua Yake

0
Kiongozi wa msafara huo, Salum Stika.

Dar es Salaam, 12 Feb 2024: Timu ya kuwawakilisha wananchi wa Zanzibar jana wameanza safari kutoka Zanzibar kuelekea Ikulu Dodoma kwa kutumia pikipiki aina ya Vespa  kwenda kumpa maua yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kumpongeza kwa mazuri aliyoyafanya pamoja na kusherehekea naye siku ya Wapendanao.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika Dar kwa boti, kiongozi wa msafara huo wa timu inayowawakilisha wakazi wa Zanzibar kwa ajili ya kupeleka maua hayo, Salum Stika amesema wameona waende kusherehekea siku hiyo wakiwa pamoja na mama.

Mmoja wa wasafiri hao kwa Vespa Bi. Khadija Saleh akielezea lengo la safari hiyo.

“Sisi kutoka Zanzibar tumeridhia na tumependezwa na uongozi wa Mh. Rais na tumeungana na Watanzania wenzetu kutoka Butiama na Arusha na maeneo mengineyo kumpa mama yetu maua yake msimu huu wa siku ya wapendanao.” Stika alimalizia kwa kusema wameamua kutumia usafiri huo ili kuonyesha utamaduni wao kwa sababu vespa ndio utamaduni wao.

Mmoja wa wasafiri hao kwa Vespa Bi. Khadija Saleh amesema kutoka na kazi kubwa anayofanya Rais ameona ni vyema kuungana na wenzao ili kuweza kwenda kumpongeza.

“Sisi Wazanzibar tumeona kazi kubwa ambayo mama anaifanya kama vile kuzingatia jinsia katika teuzi zake, amekuwa akichagua wanawake katika kuongoza kwenye nafasi mbalimbali hivyo ni mama ambaye anatambua nafasi ya mwanamke katika jamii na uongozi.

Othman Abdallah maarufu kwa jina la Makombora naye akielezea nia yake kwenye safari hiyo.

“Sasa nimeona nikampe maua yake na zawadi mbalimbali kutoka Zanzibar na tunaungana na wenzetu ambao wanatokea katika mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha,” alimaliza kusema Khadija.

Naye muendesha Vespa mwingine katika safari hiyo, Othuman Abdallah maarufu kwa jina la Makombora amesema kutokana na kazi nzuri na mafanikio ambayo Dk Samia ameyafanya ameona ni vyema kuungana kwenda kumpongeza.

Safari ya kuelekea Dodoma ilivyoanzia Dar baada ya kushuka kwenye boti ya Zanzibar.

“Tunakwenda kujumuika naye kwenye sikukuu ya wapendanao na mama kwa sababu kumuunga mkono katika jitihada zake za kutaka kutufikisha Watanzania wote kwenye kilele cha mafanikio na maisha bora, Chanda chema huvikwa pete hivyo tunakwenda kumpa mama maua yake.” Alimaliza kusema Makombora.

Leave A Reply