visa

Shilole:Mimi kuwa mjamzito, shida nini?

BAADA ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ana ujauzito, paparazi wetu alimtafuta na kumbana juu ya hilo ambapo mwenyewe alisema; ‘hata kama ninao shida iko wapi?’  Msanii huyo alisema kwa mazingira aliyo nayo sasa hata akipata mimba sio tatizo kwa kuwa kwanza siyo mtoto mdogo na pili ni mke halali wa Mr Uchebe, hivyo kuzaa kwake ni heshima ya ndoa yake.

“Hata ikiwa ni kweli nina mimba tatizo liko wapi, maana mimi sio mtoto mdogo kwamba nikiipata nitashangaza ulimwengu, lakini pia watu wajue nimeolewa na ninaishi na mwanaume hivyo hata ikiwa ninayo haiathiri jambo lolote,” alisema Shilole a.k.a Shishi Baby.

NA MEMORISE RICHARD
Toa comment