The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Droo ya 3, Aprili 26

0

ALLY KATALAMBULA | UWAZI | DAR ES SALAAM

Zikiwa zimebaki siku nane ili ichezeshwe droo ndogo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, wasomaji wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zao huku wakipewa maelekezo na Mr Shinda Nyumba pamoja na Afisa Masoko wa Global, Jimmy Haroub.

Akizungumza na Gazeti la Uwazi jana Jumatatu, Jimmy alisema kuwa mipango yote kwa ajili ya shughuli hiyo ya tatu imekamilika na kilichobakia ni kusubiri siku ifike shughuli ifanyike.

Wakati ikithibitika juu ya sehemu ya kufanyia droo hiyo inayosubiriwa kwa hamu, wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Amani, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda , waliendelea kujigamba kuwa huu ni wakati wao wa kujinyakulia zawadi.

“Najua ni bahati nasibu, lakini kujitabiria ushindi siyo jambo baya, maana ukisubiri mtu akutabirie mazuri utakaa sana, sasa naendelea kununua magazeti na kuhifadhi kuponi, kila ninapopata nafasi ninazipeleka mwenyewe ofisini Global, sitakaa mbali siku hiyo ili kushuhudia,” alisema Ally Ndufa wa Bunju jijini Dar es Salaam.

Titus Alfayo kutoka Tanga, naye alisema japokuwa atakuwa mbali siku ya kuchezwa kwa droo hiyo, ana uhakika wa kushindwa kwani uzoefu unaonyesha wanaoshinda zawadi siyo wote huwa wa Dar es Salaam, kwani katika droo ya kwanza, mshindi wa pikipiki alikuwa ni mwenyeji wa Muheza, mkoani Tanga, droo ya pili akashinda pikipiki mwenyeji wa Dar es Salaam.

“Ingawa kuwepo mwenyewe eneo la tukio ni jambo zuri, lakini sisi tunawaamini sana Global, kama ni kuponi yako ndiyo imeshinda, zawadi zako utapata tu, hivyo tunaisubiri hiyo siku kwa hamu na sisi tutakuwa tunaomba dua tu tuibuke washindi,” alisema msomaji huyo.

Bahati nasibu hiyo kubwa kabisa kuwahi kuchezwa na kampuni ya magazeti nchini, inadhaminiwa na Kilimanjaro Institute of Technology and Management iliyopo Mwenge kwa Mama Ngoma na Afrikasana na British School ambayo ipo karibu na Kituo cha Daladala cha ITV, karibu na Kanisa la Lutheran.

 

Leave A Reply