The House of Favourite Newspapers

Acha Maneno, Miliki Nyumba kwa Shilingi 500 Tu

0

shinda-nyumba-4 Wauza magazeti wakimuelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi ya Shinda Nyumba iliyoko ukurasa wa pili wa kila Gazeti linalochapishwa na Global Publishers.

Umeisikia hii! Lile Shindano la Shinda Nyumba ambalo linandeshwa na Kampuni ya Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Amani, Championi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda na Uwazi limerudi tena katika msimu wake wa pili.

shinda-nyumba-awamu-ya-pili-7

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo jana.

Baada ya miezi michache iliyopita kumshuhudia mwanamke kutoka mkoani Iringa, Nelly Mwangosi  akishinda na kukabidhiwa nyumba mpya kabisa ikiwa na samani zake zote ndani kwenye msimu wa kwanza wa shindano hilo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-9

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akizungungumza jambo wakati alipozindua Shinda Nyumba Msimu wa Pili.

Hatimaye msimu wa pili umefunguliwa wiki hii na hivyo unatakiwa kukaa mkao wa kula kwani mshindi wa msimu huu wa pili anaweza kuwa wewe.

SHINDA NYUMBA (23)Shigongo akimkabidhi mshindi wa nyuba msimu uliyopita, Nelly Mwangosi nyumba aliyoshinda.

Unachotakiwa kufanya ni rahisi tu, wewe nunua magazeti hayo yaliyotajwa juu, kwenye ukurasa wa pili utakuta kuponi ambayo utatakiwa kuijaza, kuikata na kisha kuituma kwenye sanduku la posta lililoandikwa kwenye kuponi hiyo au kumpelekea wakala yeyote aliyekaribu nawe naye ataituma kwetu au leta moja kwa moja ofisini kwetu, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam.nyumba

Nyumba aliyoshinda Nelly msimu uliyopita.

Hii ni nafasi yako, kwa shilingi 500 tu unaweza kuibuka mshindi wa nyumba hiyo iliyopo Bunju B, jijini Dar es Salaam. Acha maneno shiriki Shinda Nyumba.

Hivi Ndivyo Ulivyokuwa Uzinduzi wa Shinda Nyumba Awamu ya Pili

Leave A Reply