The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba… Pikipiki, Phantom 6, Kutolewa Kesho!

0

NA MWANDISHI WETU | UWAZI | SHINDA NYUMBA

WASHINDI wanne wa droo ndogo ya tatu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili iliyofanyika wiki iliyopita katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam, watapewa zawadi zao kesho katika hafl a itakayofanyika kwenye ofi si za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho aliliambia Uwazi kuwa watakaopata zawadi hiyo ni Agnes Lyimo wa Tanga aliyejishindia zawadi ya pikipiki, Mgaza Mwemanga wa Manzese jijini Dar aliyeshinda simu ya kisasa aina ya Phantom 6, Shaban Muhindila wa Morogoro aliyepata Seti ya Televisheni (Flat Screen) na Aveline Thomas wa Keko jijini Dar (Dinner Set).

 

 

“Tunawasihi wasomaji wa magazeti yetu ya Championi, Ijumaa, Amani, Risasi, Uwazi na Ijumaa Wikienda waendelee kukata kuponi zao kwa sababu zawadi zingine bado zipo za kutosha kabla ya bahati nasibu kubwa kwa ajili ya nyumba ambayo ipo Dar es Salaam,” alisema Mrisho.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology ambao wawakilishi wao pia watakuwepo katika hafl a hiyo na kupata fursa ya kuwaelezea wananchi juu ya ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa.

 

Leave A Reply