The House of Favourite Newspapers

‘SHINDA NYUMBA’ YATIKISA MLANDIZI

0
Wasomaji wakiwa bize kujaza kuponi za Shinda Nyumba kujaribu bahati yao ya kujishindia nyumba mpya itakayotolewa na Global Publishers.

 

BAHATI Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili leo ilitembelea eneo la Mlandizi mkoani Pwani ambako Mr Shinda Nyumba amegawa zawadi kwa mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi.

 

…Wakiendelea kujaza kuponi za Shinda Nyumba.

 

Akizungumza na globalpublishers.co.tz, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, amesema lengo la msafara huo lilikuwa ni kuwashukuru wasomaji wa maeneo hayo kwa mshikamano wao katika kuhakikisha bahati nasibu hiyo inafanikiwa.

Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub akiwaelekeza wasomaji namna ya kujaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili wa kila Gazeti la Global Publishers.

“Kama tungeweza, tungefika kila eneo kuwashukuru wasomaji wa magazeti yetu kwa sapoti kubwa ambayo wametoa katika kipindi chote hiki. Hapa tulipo tunaelekea mwishoni kabisa mwa tukio hili ambalo zawadi kubwa ya nyumba inaenda kutolewa.

Mr. Shinda Nyumba akimsaidia msomaji kujaza kuponi.

“Tukiwa Mlandizi, tumekutana na wasomaji wa Kibaha, Ruvu hadi Chalinze, kwa kutambua umuhimu wao, Mr Shinda Nyumba, yule kijana anayehisiwa kuwa ndiye mrefu kuliko wote Tanzania kwa sasa, amegawa zawadi kwa wasomaji waliokuwa wakinunua na kusoma magazeti yetu, hasa ya leo ambayo ni Ijumaa Wikienda na Championi Jumatatu, ambao wamezawadiwa hapohapo,”

Kuponi zikiendelea kujazwa.

 

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya washindi wa droo ndogo ya tano kukabidhiwa zawadi zao katika tukio lililofanyika kwenye ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa washindi waliopatikana katika droo hiyo ndogo ya tano ni Geofrey Shangalawe wa Kigoma aliyejishindia seti moja ya televisheni kubwa ‘flat screen.’

NA RICHARD BUKOS | ALIYEKUWA MLANDIZI KIBAHA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply