The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Etihad Laanzisha Usafirishaji Mizigo Kwenda Ubelgiji

0

Etihad

Shirika la Ndege la Etihad kupitia kitengo cha cha vifurushi, limeanzisha safari mbili kwa wiki ili kusafirisha mizigo  kwa kutumia ndege ya A330 itakayotoa huduma zake kwenda Uwanja wa Ndege Brussels  nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kiuchumi kati ya Abu Dhabi na Brussels na kongeza ufanisi wa huduma kwa wateja wake.

Ndege hiyo hutoa huduma ya usafiri mjini Brussels pia ikibeba mizigo, usafiri huo wa ndege ni muhimu kwa uchumi wa Ubelgiji na  Ulaya kwa ujumla.

Makamu wa Rais Kitengo cha Vifurushi wa Shirika la Ndege la Etihad, David Kerr alisema, “Brussels ni njia muhimu barani Ulaya kwa shughuli za usafiri wa ndege, ni eneo ambalo tumepanga kujitanua zaidi kwa mwaka huu, tunafurahia kuanzisha shughuli zetu ndani na  nje ya mji huu. Brussels ni kiungo muhimu barani Ulaya na kiungo muhimu kwa Afrika, hivyo tunaamini itakuwa njia muhimu zaidi ambayo itaunganisha ulimwengu katika mtandao wa usafiri wa anga.”

Ikiwa ndiyo inaoongoza barani Ulaya kwa lango la kibiashara, Uwanja wa Ndege wa Brussels utanufaika zaidi na huduma ya usafirishaji wa mizigo kutokana na kuwapo na barabara ambazo haziwezi kustahimili usafirishaji wa mizigo kwa sababu ya kuharibiwa na barafu, jambo liloloweza kuharibuvifaatiba na bidhaa zingine zisizodumu kwa muda mrefu.

Kitengo cha Vifurushi  Etihad kilizindua usafirishaji wa bidhaa za madawa ya hospitali Machi 2015. Kwa kuzingatia umuhimu wa bidhaa hizo zinahitaji umakini wa hali ya juu  na husafirishwa kwa makubaliano na viwanda husika.

Kuwapo kwa vifaa maalumu vya kupima joto kumewezesha kudhibiti kiwango cha joto linalohitajika ili kuziweka dawa hizo katika ubora unaostahili ili kuendana na mazingira ya hali ya hewa vinaposafirishwa. Programu hiyo inasimamiwa na wafanyakazi waenye uzoefu Kitengo cha Vifurushi cha Etihad huku wakisaidiana na wafanyakazi wengine.

Ndege hiyo mpya itakayosafirisha mizigo, itaunganisha masuala mbalimbali baina ya Abu Dhabu na mtandao wa  wasafirishaji wengine ulimwenguni kukiwa na takriban fursa 1,000 kwa wiki.

KUHUSU SHIRIKA LA ETIHAD

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad  ni linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya shughuli zake; kupitia Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika nane; : Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia, na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi kama  Etihad Regional.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Makao makuu yake yakiwa Abu Dhabi, Shirika la Etihad limetangaza malengo ya kuhudumia abiria 117 na mizigo Mashariki ya KATI, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 122, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa;  ikiwamo  71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s and 10 Airbus A380s

Kuhusu Uwanja wa Ndege wa Brussels

Uwanja wa Ndege wa Brussels ni miongoni mwa viwanja vikubwa vya ndege barani Ulaya, kinachohudumia takriban abiria milioni 23.5 na kubeba tani 489,00 kwa mwaka. Uwanja huo wa ndege unaunganisha miji 226 barani Ulaya na ulimwenguni kote, ukihudumiwa na ndege tofauti tofauti 77.(Takwimu za mwaka 2015.) Uwanja wa Brussels hutoa huduma zake kwa wasafiri wa daraja la kwanza huku ikiwa na gharama nafuu Zaidi nchini humo.

Uwanja wa Ndege wa Brussels ni sehemu ya pili muhimu kama kitovu cha uchumi nchini Ubelgiji kutokana na kutoa ajira takribani 60,000. Uwanja wa Ndege wa Brussels unaendeshwa na Kampuni ya Uwanja wa Ndege ya Brussels. Asilimia 25 inamilikiwa na Serikali ya Ubelgiji na  asilimia 75 ipo chini ya wawekezaji binafsi.

Tembelea… @brusselsairport katika Twitter au  www.facebook.com/brusselsairportBRU

Kwa mawasiliano zaidi;
John Greenway
SHIRIKA LA NDEGE ETIHAD
Simu: + 971 2 511 1520
Baruapepe:[email protected]

Leave A Reply