The House of Favourite Newspapers

Shoga; mumeo siyo kaka yako, usimuonee aibu!

0

hotsexylady94968Shoga, matumaini yangu kwamba hali yako ni nzuri na ulisherehekea vizuri Sikukuu ya Idd na Krismasi na sasa unajiandaa kuupokea Mwaka Mpya wa 2016.

Kama sikukuu hizo hazikuwa nzuri kwako, hebu jipange ili Mwaka Mpya nawe ufurahi kama ilivyokuwa kwa wenzako ambao walifurahi kuwa na wenza wao wakila na kunywa.
Leo shoga yangu nataka kuzungumza na wewe kuhusu tabia ya kumuonea aibu mumeo wakati siyo kaka yako wala mkweo.

Nasema hivyo kufuatia mazungumzo yaliyojiri baina yangu na mwenzetu mmoja aliyenichekesha na kunishangaza aliponifahamisha kwamba huwa anamuonea aibu mumewe.

Mwenzetu huyo aliniacha hoi aliponieleza kwamba, kutokana na aibu hata ‘mista’ wake anapojisevia ‘tunda lake’ mchana hujifunika kanga au mtandio usoni na usiku huzima taa.

Awali nilifikiri ananitania lakini baada ya kumbana akaniambia niamini maneno yake hapo ndipo nikabaini wapo shoga zetu wengine wenye tabia hiyo.Shoga, sasa unapomuonea aibu mumeo aliyekutoa kwenu na kukupeleka kwake kwa ajili ya kazi moja tu kumpa raha na kumzalia, inakuwaje?

Nini kinachokufanya umuonee aibu maana raha ya mapenzi ni kwa wahusika kuachiana miili yao ili kila mmoja acheze na mwili wa mwenzake kwa raha zake.

Pia mapenzi hunoga hasa baba anapomuangalia mkewe jinsi macho yalivyomlegea au mtoto wa kike alivyoumbika kwa kuwa na nido nzuri, hipsi za kimashamshamu nk.
Aidha, kwa mama kukiangalia kifua kipana cha mumewe kilichopambwa na vinyweleo laini, alivyojaaliwa na maeneo mengine.

Shoga, kama una tabia ya kumuonea aibu mumeo hebu iache, jiachie kwake mwanzo mwisho kwa sababu siyo kaka yako au mkweo na kama usipobadilika siku atakayokutana na mwenzako asiye na aibu atahamia kwake jumla.

Leave A Reply