Shoga; Ukiwa Mbunifu Mumeo Hatachepuka Nje

loveShoga, yangu kadiri siku zinavyo-kwenda ndivyo joto la uchaguzi linazidi kupanda kwani tumebakiza siku… kabla ya kutumia vikatio vyetu kuwakata viongozi wasiofaa na kuwachagua wanaofaa.

Ni imani yangu kwamba kufikia leo mmekwisha sikiliza sera za wagombea udiwani, ubunge na urais na kuwajua wagombea wanaofaa kutuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Cha msingi siku ya kupiga kura mjitokeze kwa wingi kwenye vituo.

Shoga baada ya kuzungumza nanyi kwa kifupi kuhusu uchaguzi, narejea kwenye jambo nililowaandalia linalohusu ubunifu kwani kila kitu kinachofanyika chini ya mbingu ili kiweze kufanikiwa kinahitaji ubunifu.

Kama wewe ni mfanyabiashara, mkulima, mwanamichezo, mwanajeshi, mwalimu, fundi ujenzi, fundi magari, mpishi, msusi, polisi, fundi seremala, fundi cherehani, mcheza filamu na hata kama ni mwandishi wa habari kama nilivyo, bila kuwa mbunifu ni kwamba utakwama.

Nasema hivyo kwa sababu dunia ya leo ukitaka kupata mafanikio ubunifu unahitajika kwa asilimia mia moja, kinyume chake utahisi unarogwa kumbe unajiroga mwenyewe kwa kukosa ubunifu.

Tukija katika mambo yetu ya chumbani zaidi, ubunifu unahitajika sana tena bora uzembee kwenye kazi unayofanya kuliko kutokuwa mbunifu kwenye eneo hilo linalohusu mapenzi ambayo yametawala dunia.

Shoga, kila siku unatakiwa kuwa mbunifu wa mapenzi kuhakikisha mumeo anafurahi kuwa nawe mnapokuwa kwenye uwanja wa fundi seremala na mkishamaliza kufanyiana mambo yenu ya chumbani zaidi afungue droo na kutoa pochi yake kisha akupatie fungu la kutosha ukanunue chochote ulichopungukiwa.

Kama ulikuwa huna utamaduni wa kuangua kilio wakati anakushika hapa na pale, anza kulia mwanakwetu huku ukimuita kwa majina yake yote na kumsifia kwa jinsi anavyokufurahisha.

Shoga, kama huwa unapenda kutumia mtindo mmoja tu, hebu mbadilishie uone atakavyokusifia, kama ulikuwa hujui ni nguo gani ukivaa zinahamasisha akuhitaji hata kama alikuwa hana mpango wa kula tende zake, anza kumvalia nguo za mitigo mkiwa chumbani, huo ndiyo ubunifu ninaouzungumzia.

Kwa kifupi shoga yangu unapaswa kuwa mbunifu kila idara ili kumfanya mumeo akuwaze wewe na kutofikiria michepuko ya nje ambayo hutumia ubunifu kuwanasa waume za watu na siyo limbwata kama wengi wanavyodai kwani mapenzi ni utundu na siyo uchawi. Bye!

Toa comment