The House of Favourite Newspapers

Shoga; umeolewa, ofa ya masela yanini?

0

Vanessa3Shoga yangu, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu mimi sijambo pamoja na familia yangu akiwemo shemeji yenu ambaye ndiyo kila kitu kwangu.Shoga yangu, leo nazungumza nawe kuhusu ofa, ofa haina tatizo kabisa kwa sababu mtu anayekununulia kinywaji au chakula huyo anakujali na kukuthamini.

Japo kuna ofa za aina nyingi lakini leo nitazungumzia ofa ya kilevi, nyama choma na mchemsho ambayo imekuwa ikipendwa sana hususan na wanawake ambao huwa wanapasha yale maji ya dhahabu.
Siyo vibaya mwanamke kupewa ofa na watu wake wa karibu kama mashemeji, wadogo zao, majirani lakini inatia shaka pale mama aliyeolewa kila siku anapokuwa baa akipata bia za ofa.

Utamuona mama huyo ikifika jioni bila kujali kama ameolewa na ana familia, anakwenda baa kwa ajili ya kupata ofa ya kinywaji aliyopewa na kijana wa mtaani maarufu kama msela.Kutokana na tabia hiyo, anajiachia huko bila kujali kama mumewe ambaye hanywi pombe anaboreka kiasi gani na wala hajui kinachoendelea kwa watoto wake.

Kama unavyoelewa watu wanavyobadilika tabia baada ya kupata kilevi, mama huyo akilewa unaweza kukuta akishikwashikwa mwilini na wengine hujikuta wakizisaliti ndoa zao.Shoga yangu, hivi unajisikiaje mama uliye kwenye ndoa kuendekea ofa ya kilevi ambayo mwishowe inakutoa ufahamu na kufanya mambo ya aibu?

Kumbuka mwanamke yeyote ni mlezi wa familia na jamii kwa ujumla, hivyo unapaswa kujiheshimu na kuacha kuendekeza tabia ya kupenda kilevi kupita kiasi.Hata kama wewe ni mwana chama wa yale maji ya dhahabu, kuwa na kiasi na ikiwezekana unapopewa ofa muwe na mumeo.

Leave A Reply