The House of Favourite Newspapers

Shoga; usimpangie mumeo ratiba ya malovee!

0

shutterstock-couple-hugging

Shoga yangu, kwa mapenzi ya Mola ni matumaini yangu kwamba afya yako ni njema na mapambano ya maisha na malezi ya familia yanakwenda vizuri.

Kwa upande wangu nipo vizuri, naendelea kulisongesha mbele gurudumu la maendeleo ya taifa letu pamoja na kuwaandalia ‘topiki’ kama hii ya leo.

Leo shoga yangu nitazungumzia ishu inayofanywa na baadhi ya wenzetu ya kuwapangia ratiba waume zao ya kula chakula cha usiku a.k.a tende.

Nimekuja na mada hii baada ya shemeji yangu sitapenda kumuanika jina kunifuata na kunilalamikia juu ya mkewe kumpangia ratiba ya kula tende.

Shemeji yangu huyo alinieleza alitaka kutafuta mchepuko kwa ajili ya kukata kiu yake lakini baada ya kufikiria sana suala la maradhi ndiyo kaamua kunieleza ili nikazungumze na mkewe.

Shoga yangu, kufuatia kesi hiyo nimebaini wapo wenzetu wengi wanaowafanyia hivyo waume zao, kwa mujibu wa shemeji yangu yeye kapangiwa ratiba ya kula tende siku ya Ijumaa na Jumamosi tu.

Anasema anapozihitaji tofauti na siku hiyo hapewi, hakika ni jambo la kushangaza sana na linahatarisha maisha ya ndoa.

Shoga yangu, suala la chakula cha usiku halina muda labda kwa sababu maalum na kila mmoja aridhishwe nayo tofauti na hapo utakuwa unakosea kumpangia ratiba mumeo.

Hivi mumeo akitafuta nyumba ndogo utamlaumu au utaenda kumshtaki kwa nani? Hebu acha tabia hiyo kwani hata katika vitabu vitakatifu imeandikwa mama au baba wasinyimane kupeana haki ya ndoa na jambo hilo ndilo linalowaunganisha.

Leave A Reply