The House of Favourite Newspapers

Simanzi! Mazishi ya Kaka wa Mpiga Picha Mkuu wa Global – Pichaz

Richard Bukos akipita kuaga mwili wa kaka yake, nyumbanin kwao, Kigogo Ruhanga.

MPIGA Picha Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Amani, Championi, Spoti Xtra na Betika, Richard Bukos amepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kaka yake, Samson Bukos aliyefariki dunia juzi, Alhamisi, Machi 21, mwaka huu katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam.

Mwili ukiwasili nyumbani.

Mwili wa Samson umezikwa leo, Jumamosi, Machi 23, 2019 katika makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam ambapo wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho wameungana na ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wengine kuwafariji wanafamilia ya Bukos, nyumbani kwao, Kigogo Ruhanga.

Wakati wa kuaga mwili wa Samson, simanzi, majonzi, na vilio vimetawala kwa ndugu na watu wa karibu wa marehemu kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa ndugu yao huyo ambaye amefariki ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi hali iliyosababisha mama wa marehemu kuishiwa nguvu.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiaga mwili wa Samson Bukos.

Aidha, katika ibada fupi ya kuaga na mazishi ya mwili wa marehemu, iliyoongozwa na Mchungaji Hasheem Atilio wa Nazareth Miracle Church amesema kuwa Samson Bukos amepumzika na waliobaki wanapaswa kumrudia Mungu na kutenda mema ya kumpendeza Mungu angali wakiwa hai kwani siku ya mwisho kila mwanadamu atahukumiwa kulingana na matendo yake.

Mfanyakazi wa Global, Laurian Lutambi akiaga mwili wa marehemu.

“Ni heri kumkumbuka Mungu ukiwa baa unakunywa bia, kuliko kumkumbuka mchepuko wako wakati ukiwa kanisani kwenye ibada,” amesema Mchungaji Atilio.

Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akiaga.

Pia, mchungaji huyo ameitaka familia ya Bukos kutohuzunika sana kwani marehemu alimwamini Mungu, hivyo wamuombee ili Mwenyezi Mungu ampokee peponi.

Mama marehemu, Esther Bukos akiaga mwili wa mwanaye.

 

Mkuu wa Idara ya Global Digital, Edwin Lindege akiaga.

 

Mkuu wa Idara ya Uhasibu wa Global Publishers, Lawrence Kabende akiaga.
Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Richard Manyota akiaga.

 

Samson Bukos enzi za uhai wake.

 

 

 

 

Wafanyakazi wa Global wakimpa pole, Richard Bukos kwa kuondokewa na kaka yake.

 

Mchungaji Hasheem Atilio wa Nazareth Miracle Church  akitoa neno wakati wa ibada ya mazishi.

 

 

Richard akiweka shada kwenye kaburi la kaka yake.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHRERS

Comments are closed.