The House of Favourite Newspapers

Simanzi na Huzuni Kuagwa kwa Mwili wa Mama wa Sugu – Picha + Video

Mwili wa marehemu ukitolewa kanisani baada ya kuagwa.

SIMANZI na huzuni vimetawala wakati wa kuaga mwili wa mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), Bi. Desderia Lungu Mbilinyi leo Jumanne, Agosti 28, 2018 katika Kanisa Katoliki lililopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Mtoto wa marehemu, Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Suhu’ akiaga mwili wa mama yake mzazi.

Bi. Desderia Mbilinyi alifariki dunia juzi Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) akipatiwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka wodi namba 18 kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Mjukuu wa Marehemu ambaye ni mtoto wa Sugu na Faiza, Sasha akiaga mwili wa bibi yake.

Viongozi Mbalimbali wa Serikali, vyama, dini, siasa, ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza Muhimbili kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa mama Mbilinyi.

Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenza Mbeya kuzikwa.

Miongoni mwa viongozi waliungana na familia na waombolezaji ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, baadhi ya wabunge ambao ni Halima Mdee wa Kawe, Ester Bulaya wa Bunda, na mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Fredy Lowassa na wengine.

Baada ya kuaga mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda nyumbani kwake, jijini Mbeya kwa ajili ya maziko.

Msanii wa Hip Hop, Kala Jememaya akiaga mwili wa mama yake Sugu.
Mbunge, Halima Mdee akiaga mwili wa marehemu.

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akiaga mwili wa marehemu.

Na Edwin Lindege, Picha Zote na Denis Mtima | GPL

====

FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA KUPITIA GLOBA TV ONLINE

Comments are closed.