The House of Favourite Newspapers

Simanzi Yatawala Mazishi ya Bilago, Kigoma – Pichaz

 

SIMANZI na majonzi vimetawala wakati wa mazishi ya mwili wa aliyekuwa mbunge wa Buyungu (Chadema), Kasuku Samson Bilago aliyezikwa jana katika makaburi ya Kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma apikozaliwa.

 

 

Shughuli ya mazishi hayo iliznza kwa ibada ya misa ya mazishi katika Kanisa Katoliki Kigango cha Kasuga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla ya kuelekea makaburini kwa maziko.

 

 

Wakati wa shughuli hiyo, vilio, simanzi na majonzi vilitawala kwa wakazi wa Kasuga, ndugu, marafiki,  wanachama na wafuasi wa Chadema wakati mwili huo ulipowasilishwa kanisani na baadaye kupelekwa makaburini.

 

 

Waliopata nafasi ya kumzungumzia Bilago, wengi wao walisema marehemu alikuwa akiishi maisha ya kijamaa na wananchi wa jimbo lake la Buyungu na kila sehemu aliyofanya kazi ikiwemo bungeni na fani yake ya ualimu.

 

Bilago aliwahi kuwa mwalimu na baadaye Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Mbeya kabla ya kuingia kwenye siasa.

 

 

Bilago ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, alifariki dunia Jumamosi iliyopita, Mei 26, 2017 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akipatiwa matibabu

 

Bilago alizaliwa Februari 2, 1964 na alikuwa mwanachama wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta.

 

PICHA: CHADEMA MEDIA

Comments are closed.