The House of Favourite Newspapers

Rais JPM Atangaza Maombi Siku 3 “Tusitishane” – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kuliepusha Taifa la Tanzania dhidi ya Ugonjwa wa Corona na kusisitiza kuwa hatatangaza Lockdown.

 

 

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akiongoza waombozaji kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19,2021.

 

 

“Tusitishane na kuogopeshana Mungu yupo, Mungu ndiyo muweza wa yote, Tuendelee kusimama na Mungu, tulishiinda Corona mwaka jana. Naomba Tusimame na Mungu, “,amesema Rais Magufuli.

 

 

“Magonwa yapo na yataendelea kuwepo, magonjwa ya vifua, magonjwa ya kupumua yapo. Kufa tutakufa tu, unaweza ukafa kwa Malaria, Kansa na Magonjwa mengine, kufa kupo, ila kamwe tusimuache Mungu, Waislamu walitangaza muda wao wa kuomba, Waislamu wameanza leo, kesho Wasabato, Jumapili Wakristo kwa siku 3 kwa kuomba na kufunga tutashinda.

 

“Naomba Watanzania kama kuna mahali tumetetereka tumuombe Mungu. Mungu ndiyo mwenye uwezo wa kila kitu, viongozi wa dini endeleeni kusisitiza maombi, tumeshinda mwaka jana na sasa naomba tuendelee kumuomba Mungu”,amesema

 

“Hatutaweka Lockdown kwa sababu Mungu Muda wote yupo. Taifa hili lipo mikononi mwa Mungu na Mungu ataendelea kusimama nasi,” amesema Rais Magufuli.

 

Leave A Reply