The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Wahitimisha Chemsha Bongo ya Spoti Xtra

0
Maua Mutabazi (kulia) akipokea zawadi yake kutoka kwa Mtangazaji wa +255 Global Radio na Global TV Online ambaye pia ni mwakilishi kutoka Vunja Bei Mobile Shop, Kissa Daniel.

ILE Chemsha Bongo iliyokuwa inaendeshwa na Gazeti la Spoti Xtra ambayo ilikuwa inawapa fursa wasomaji wa gazeti hilo kujishindia zawadi mbalimbali kama seti za vyombo, microwave, friji na vyombo mbalimbali vya nyumbani, imefikia tamati leo Jumanne baada ya washindi watatu kujishindia zawadi mbalimbali.

 

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Lucy Mgina akimkabidhi Gaisa Hamis zawadi yake.

 

 

Washindi hao watatu waliohitimisha chemsha bongo hiyo na kukabidhiwa zawadi zao jana Jumanne kwenye Ofisi za Gazeti la Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori jijini Dar ni Maua Mutabazi ambaye ni shabiki wa Simba kama ilivyo kwa Gaisa Hamis pamoja na Mwanaidi Ally, shabiki mkubwa wa Yanga.

 

Mwanaidi Ally akipokea zawadi yake kutoka kwa Mhariri Msaidizi wa Championi Ijumaa, Said Ally.

 

Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunja Bei Mobile Shop ilianzisha chemsha bongo hiyo ambayo ilidumu kwa takribani miezi mitatu kuanzia Desemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu, lengo kubwa ni kuwaleta karibu wasomaji wake huku pia ikiwa ni ujio wa Gazeti la Spoti Xtra Jumanne.

 

Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri na mwandishi wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra, Hussein Msoleka (wa pili kushoto).

 

 

 

Kwa sasa Gazeti la Spoti Xtra linapatikana mtaani mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI kwa bei ya Sh 500 tu.

 

STORI: HUSSEIN MSOLEKA
PICHA: MUSA MATEJA

Leave A Reply