The House of Favourite Newspapers

Simba Yatua Kwa Mzambia Samuel Sikaonga

0

KIUNGO mkata umeme wa Zesco ya nchini Zambia, Samuel Sikaonga, ameweka wazi kuwa mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu Bara, Klabu
ya Simba wametuma ofa wakitaka ajiunge nao.

 

Mbali na Simba, Sikaonga amesema pia Azam FC wametupa ndoano kwake wakitaka ajiunge nao kwenye dirisha
dogo lililofunguliwa juzi
Jumatano.


Kiungo huyo mkabaji
mwenye miaka 22, ameliambia ChampioniIjumaa kuwa, amepewa taarifa
na viongozi wake kuwa Simba
na Azam FC zinamtaka na yeye yuko tayari kujiunga na timu moja wapo itakayokuwa na ofa nzuri.


“Ni kweli nimeambiwa na
uongozi wangu kuwa Simba na Azam wananihitaji na mimi nipo tayari kuweza
kujiunga nao, maana Simba
ni timu nzuri pia Azam ni wazuri ni suala la muda,” alisema kiungo huyo ambaye
ana mkataba wa miaka miwili
Zesco.


Akizungumzia ishu ya
usajili, Simba kupitia Kocha Msaidizi wao, Thierry Hitimana alisema kuwa:
“Najua kuna wachezaji lazima
wataongezwa ila mpaka sasa bado sijaambiwa ni nani na nani nafikiri kocha mkuu, Pablo (Franco) ataongea na uongozi ilo suala la usajili tutaliweka wazi baadaye.”

MAJANGA SIMBA: ROBO TATU YA WACHEZAJI SIMBA WANAUMWA KOCHA AFUNGUKA “TUMEWAACHIA MADAKTARI…”

Leave A Reply