The House of Favourite Newspapers

Simba Yawapangia Mtibwa Full Mkoko

0

KIKOSI cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kimeondoka jana asubuhi kuelekea mkoani Morogoro kikiwa kamili tayari kuwavaa Mtibwa Sugar kesho Jumamosi.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kutokana na kila upande kupania kuvuna pointi tatu.Katika mchezo uliopita wa ligi, Simba ilifanikiwa kuvuna pointi tatu kwa kuwafunga Ihefu FC mabao 2-1 huku Mtibwa yenyewe ikitoka suluhu na Ruvu Shooting.

Akizungumza na Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema wachezaji wao wote 28 waliosajiliwa kwa ajili ya msimu huu wapo tayari kuwavaa Mtibwa.

 

Rweyemamu alisema mara baada ya kutua mkoani huko jana, wanatarajiwa kufanya mazoezi kwa siku mbili ili wachezaji wao wazoee mazingira kabla ya kushuka uwanjani kucheza na Mtibwa.

Aliongeza kuwa msafara huo umewahusisha wachezaji Luis Miquissone, Gerson Fraga, Chris Mugalu, na Pascal Wawa walioachwa kwenye safari ya Mbeya timu hiyo ilipokwenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

“Kikosi chetu kimeondoka leo (jana) asubuhi kikiwa na wachezaji wetu wote 28 tuliowasajili kwa ajili msimu huu wa 2020/21, hiyo katika kuhakikisha timu inapata ushindi.“Maandalizi katika kuelekea mchezo huo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri ya kuhakikisha tunaendelea na ushindi kama tulioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Ihefu,” alisema Rweyemamu.

Stori: Wilbert Molandi,Dar es Salaam

Leave A Reply