Simulizi Ya Santi Cazorla Hadi Huruma!
KARIBU mwaka mmoja na nusu yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha. Huyu ni kiungo wa Arsenal, Mhispaniola, Santi Cazorla, lakini pamoja na ufundi wake, ameshindwa kabisa kucheza.
Achana na majeraha, lakini simulizi ya mateso ambayo kiungo huyo alipitia katika kipindi kigumu cha kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu, ndiyo ambayo inawasisimua na kuwahuzunisha wengi.
Cazorla, juzi alizungumzia mateso aliyopitia na hakika ni simanzi kubwa.
Fundi huyu ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Arsenal, alichanwa mguu mara nane ndani ya mwaka mmoja, kwa maana ya kufanyiwa oparesheni ili kujaribu kutibu tatizo linalomsumbua.
C a z o r l a ameeleza kuwa ilibaki kidogo tu akatwe mguu na kuanza k u t e m b e l e a fimbo kutokana na kuingiliwa na kirusi ambacho k i n g e w e z a kuhat ar i sh a maisha yake. Tangu hapo, alisu bir i miujiza tu kama anaweza tena kucheza soka.
Lakini kutokana na kukatwa sana mguu katika oparesheni, ngozi yake ya mguuni ilipungua, ndipo ikalazimika atolewe ngozi kidogo ya mkononi na kuwekewa mguuni.
Mhispania huyo hajaingiza miguu yake uwanjani tangu Oktoba, mwaka jana, na ililazimika afanyiwe upasuaji mara nyingi sana, hivyo kupoteza ngozi katika kifundo chake cha mguu wa kulia.
Picha alizozitoa kwa Gazeti la Marca la nchini Hispania lililomfanyia mahojiano, ambazo zinaonyesha jinsi anavyopitia kipindi kigumu, ndizo zilizowashtua wengi na kuona kumbe ilikuwa asicheze tena soka!
Picha hizo zinaonyesha madhara makubwa yanayoonekana mguuni, baada ya oparesheni nane ndani ya mwaka mmoja.
Zinaonesha jinsi ngozi yake i l i y o k u w a na tatuu katika mkono wa kushoto, sasa ikiwa imehamia kwenye kifundo cha mguu.
Ma d a k t a r i wamemwambia nyota huyo mwenye miaka 32 kuwa ana bahati k u w e z a k u t embea tena bustanini na mtoto wake, huku pia ikionekana kuwa miujiza, kwamba anarejea dimbani mwanzoni mwa Januari.
Cazorla aliliambia Marca: “Kama umeweza kutembea tena na mwanao bustanini, ridhika, waliniambia.”
“(Dr Mikel Sanchez) aliona kwamba nina kirusi ambacho kimekula sehemu ya mfupa katika kifundo cha mguu. Kuna sentimita nane ambazo hazikuwepo!
“Siruhusiwi kucheza hadi Januari, lakini nitarudi uwanjani kufikia muda huo.”
Cazorla anaendelea na matibabu katika mji wa kwao, Salamanca nchini Hispania lakini kocha Arsene Wenger hivi karibuni alisema yupo tayari kumkaribisha tena kiungo huyo fundi katika kikosi chake baada ya Krismasi.
Wenger alisema: “Dalili za kwanza ni nzuri, lakini hajacheza kwa karibu mwaka mmoja na nusu.
“Bado hajaanza mazoezi kamili, anahitaji mechi chache katika kikosi cha wachezaji wa akiba. Kwa hiyo, nadhani kama mambo yote yatakwenda vizuri, itakuwa ni baada ya Krismasi.”
Cazorla alijiunga na Arsenal akitokea Malaga mwaka 2012, na ameshacheza mechi 129 za Ligi Kuu England, akiwa amebeba makombe mawili ya FA.