The House of Favourite Newspapers

Wanachama 12 wa Chadema Wafikishwa Makamani Arusha

0
Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe.

Wanachama 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha leo.

 

Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper.

 

Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Leave A Reply