The House of Favourite Newspapers

Singida Kinara Matokeo ya Mtihani Kidato cha Sita 2021

0

Mkoa wa Singida umetajwa kuwa kinara wa matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei 2021.

 

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde amesema mkoa huo umefanya vizuri kwa ufaulu wa asilimia 73.91.

 

Msonde pia ameutaja Mkoa wa Lindi kwa kushika nafasi ya pili ikiwa na asilimia 73.58, huku mkoa wa Mara ukishika nafasi ya tatu kwa asilimia 72.08.

 

Vilevile, Mkoa wa Mara umekuwa mkoa wa kwanza kuongeza ufaulu wake kwa miaka mitatu mfululizo kwa asilimia 4.80 ikifuatiwa na mkoa wa Kaskazini Pemba kwa asilimia 4.46 na mkoa wa Katavi ufaulu wake umeongezeka kwa asilimia 2.77.

 

Matokeo ya Mtihani Kidato cha Sita, Ualimu 2021

Leave A Reply