The House of Favourite Newspapers

Siri Imevuja… Mrembo Amhenyesha Mondi Miaka 9

0

IMENICHUKUAmiaka tisa kumfukuzia!” Hii ni kauli ya supastaa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimzungumzia mrembo wake mpya aitwaye Andrea Abrahams, chanzo cha ndani kimelipnyezea IJUMAA mchongo mzima.

 

Diamond au Mondi amempa sifa zote akisema; ‘huyu ndiye sahihi!’Gazeti la IJUMAA linafahamu kutoka kwa vyanzo vyake vya uhakika ndani ya familia ya Mondi kwamba, jamaa huyo ana kifaa kipya na ilimchukua miaka takriban tisa kumsomesha mrembo huyo hadi akaingia kwenye kumi na nane za ‘Mzee Baba’.

 

WALIKUTANA 2013

Vyanzo hivyo vimeling’ata sikio Gazeti la IJUMAA kwamba, kwa mara ya kwanza, Mondi alikutana na Andrea mwaka 2013; wakati huo alikuwa bado hajazaa na mwanamama Zarinah Stori: Mwandishi Wetu, DARHassan ‘Zari The Boss Lady ’ ambaye amezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Ukiacha habari hizo za ndani ambazo ndizo zinazozungumzwa zaidi kwa sasa ndani ya familia ya Mondi, wawili hao hivi karibuni walikuwa kwenye mazungumzo ya ‘live’ kwenye Instagram ambapo ugha ya miili yao (body language) zilia kueleza kwamba, wawili hao ni kitu na boksi na kila mmoja amenasa kwa mwenzake.

 

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya uhakika, Mondi alianza kumfukuzia Andrea tangu mwaka 2013 na hakukata tamaa hata kidogo pamoja na kwamba hapo katikati aliruka na kuzaa na wanawake wengine, lakini Andrea aliendelea kubaki kwenye mtima wake, akiamini kwamba ipo siku atanasa kwenye ndoano na kweli leo amenasa!

NI MWANAMITINDO WA SAUZI

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umejiridhisha kuwa, Andrea ni bonge la mwanamitindo maarufu wa nchini Afrika Kusini au Sauzi.Mbali na kuwa mwanamitindo, pia anashikilia cheo cha Miss Mamelodi Sundowns Mpumalanga na Miss 7 Continents kwa mwaka 2016.

 

Ubuyu wa Mondi kuruka na mrembo huyo zilianza kusikika mara tu baada ya jamaa huyo kurejea Bongo mwishoni mwa mwezi uliopita akitokea Afrika Kusini ambako alikuwa huko kwa wiki nne, akiandaa albam yake mpya ambayo itaruka hewani baadaye mwaka huu.

 

ANDREA AVAA KOTI LA MONDI

Taarifa zaidi ziliendelea kusambaa kama moto wa kifuu baada ya mrembo huyo kuonekana akiwa amevaa koti kubwa la Mondi alilokuwa amevaa wakati akiwa nchini humo Afrika Kusini.Wawili hao; Mondi na Andrea ni marafiki kupitia Mtandao wa Instagram kwani kila mmoja amem-follow mwenzake.

AMUOMBEA TUZO BET

Tetesi hizo zimezidi kushika kasi kufuatia mrembo huyo kuapa kumfuata Mondi popote atakapokuwa.“Nitakuwa nyuma yako muda wote,” aliandika mrembo huyo katika moja ya picha za Mondi akimuombea ashinde Tuzo ya BET ambazo zitatolewa wiki ijayo huko Los Angeles nchini Marekani.“Kuna mtu ameniuliza leo mimi na wewe tulikutanaje?”

Anasikika Andrea akimwambia Mondi katika moja ya video zao.Katika majibu yake, Mondi anaonekana na kusikika akisema; “Sijui…” Kisha anaondoka hewani huku akimmwagia mabusu kama yote.Mrembo Andrea anaibuka kwenye maisha ya Mondi ikiwa ni miezi kadhaa tangu ilipoaminika kuwa anamiliki kifaa kutoka Ethiopia.

 

Miezi kadhaa iliyopita, Mondi alinaswa na mrembo huyo wa Ethiopia huku kukiwa na madai mazito kwamba huwenda ndiye angeolewa na staa huyo anayewania Tuzo ya BET.

 

ANDREA KAMA TANASHA

Andrea anatajwa kuwa na sifa za kimaumbile na rangi ambazo Mondi huwa anapendelea akifananishwa na Tanasha Donna hivyo kuna uwezekano mkubwa akaolewa na jamaa huyo ambaye ametangaza kuoa mwakani.Hadi sasa, Mondi ana kijiji cha wanawake aliotoka nao huku akizaa na watatu ambao ni Zari, Hamisa Mobeto na Tanasha.

Stori: Mwandishi Wetu, DAR

Leave A Reply