The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (20)

0

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (20)

 

ILIPOISHIA JANA…

“Karibu mpaka ndani bwana mdogo,” mzee alinikaribisha. Nami nikajimwaga katika kiti kimoja cha mbao, huku nikiliacha jicho liichunguze nyumba ile. 

 

ENDELEA KUISOMA…

Ilikuwa ni nyumba yenye vyumba vitatu na sebule. Kila kitu kilikaa hovyohovyo hata panya na popo walikuwa ni miongoni mwa wakazi wa nyumba hiyo. Ukimwondoa mzee, popo na wale panya, wakazi wengine niliowashuhudia walikuwa: nzi, mende, kunguni, chawa, viroboto, mbu na mijusi wakubwa waliotukana matusi kwa kutikisa vichwa!

 

“Haya eleza kisa cha kunifuata mpaka katika nyumba hii waiogopayo watu!” mzee alichokoza mada, akiwa naye kakaa juu ya kiti cha mbao kama nilichokalia. Tukawa tukitazamana kwa jicho la pembeni.

 

“Mzee nashukuru kwa nafasi hii! Nina matatizo mzee wangu, nisamehe kwa makosa niliyofanya… mtu wako wa ajabu hunifukuza siku zote mpaka maisha yangu yamebadilika, nashindwa hata kufanya kazi! Nisamehe kwa makosa niliyofanya na naomba uniondolee adhabu hii.”… BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Leave A Reply