The House of Favourite Newspapers

Sitti Mtemvu aibuka kampeni za Fella

0

Gladness Mallya

MISS Tanzania 2014 aliyevua taji kutokana na skendo ya kudanganya umri, Sitti Mtemvu juzikati aliibuka na kuwa kivutio kwenye kufunga kampeni za udiwani katika kata ya  Kilungule, Temeke jijini Dar anakogombea bosi wa lebo ya muziki ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella.

Ishu hiyo ilitokea Jumapili iliyopita ambapo Sitti akiwa na mama yake walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa kwenye mkutano huo wa mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliohudhuriwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho ndani ya viwanja vya Kilungule jijini Dar es Salaam.

 “Mh, umemuona Sitti jamani? Sijui wakoje na Fella mpaka amekuja huku, nilikuwa natamani sana kumuona kwani nilikuwa namsikia tu kwenye vyombo vya habari, hatimaye leo nimemuona ukweli nimefurahi sana,” alisikika mama mmoja akimwambia mwenzake.

Akizungumza na gazeti hili, Sitti alisema alifika viwanjani hapo kumsapoti Fella kwani baada ya mama yake (Fella) kufariki dunia, wazazi wa Sitti ndiyo walikuwa walezi wake. Alidai mbali na hivyo, pia ni mwanasiasa mwenzake, japokuwa yeye alishindwa kupita kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni za ubunge wa Viti Maalum mkoani Morogoro hivi karibuni.

Licha ya Sitti, mastaa mbalimbali wa muziki walitoa burudani kwenye mkutano huo akiwemo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Yusuf, MwanaFA, Shetta, Yamoto Band na wengine kibao.

Leave A Reply