The House of Favourite Newspapers

SIYO SIRI HATA STEVE NYERERE AMECHOKA!

KOMEDIANI wa Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anaamini kuwa, soko la sinema za Kibongo haliwezi kubadilika kama sura za waigizaji ni zilezile za kila siku ambazo hata yeye amezichoka.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Steve alisema kuwa, kama kila mtu anapotazama sinema anakutana na sura ya Kajala Masanja, Shamsa Ford, Aunt Ezekiel na wengine, watu wanachoka na mwisho wa siku ndipo linatokea anguko la sinema kama lilivyotokea.

Steve alisema kuwa, inatakiwa ufike wakati wale mastaa wakubwa waachie ngazi na kuwapa nafasi wengine ili watu waone ladha tofauti maana sura zao zimechosha mashabiki.

“Ninachokipigania ni kwamba waigizaji wakubwa wabaki na haki miliki zao, lakini sura za mastaa haohao zinachosha maana hata mimi nimezichoka,” alisema Steve.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.