The House of Favourite Newspapers

SNOOP DOGG APATA MJUKUU WA KIKE

Image result for snoop dog AND HIS GRAND DAUGHTER

MKONGWE wa Muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Snoop Dogg amepata mjukuu wa kike akiwa na umri wa miaka 46, baada ya awali kupata mjukuu wa kiume aliyefahamika kwa jina la Zion Kalvin kutoka kwa mtoto wake Corde Broadus.

Snoop ameposti video hiyo ya mjukuu wake wa kike huku akiongea kwa furaha kuwa ameletewa mjukuu mzuri na kukiri kuwa ni baraka waliyopata kwa mara nyingine tena “Mjukuu wangu wa kwanza wa kike hakika hii ni baraka hebu muone alivyo mzuri hongera mwanangu umefanya kazi nzuri. Asante kwa zawadi ya mjukuu tena.” Alisikika akiongea Snoop Dogg

Comments are closed.