The House of Favourite Newspapers

Snura ahama uswazi, afanya dua!

0

snura dua (3)
Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi.

Hamida Hassan na Gladness Mallya

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akiishi uswahilini huko Mwananyamala ndanindani, sasa amehamia mitaa ya kishua, sehemu za Kinondoni Mahakamani, jijini Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko lina ishu nzima.

snura dua (4)…Wakifanya dua

Snura, staa wa Wimbo wa Majanga, alikuwa mmoja wa wasanii waliozunguka na Rais John Pombe Magufuli, wakati wa kampeni za kumuuza mgombea huyo wa CCM katika mikoa mbalimbali nchini.

Katika nyumba hiyo nzuri yenye hadhi yake, siku moja tu baada ya kuhamia, Snura aliomba dua kumshukuru Mungu kwa kile alichosema kushukuru kwa kupata fedha na kumlinda kwa kipindi chote cha kampeni kilichowafanya kutumia muda mwingi safarini.

“Kutokana na safari kuwa ndefu, tena kuzunguka kwa magari sehemu mbalimbali na kurudi salama nimeona nimshukuru Mungu kwani si jambo la mchezo,” alisema Snura, akizungumzia uamuzi wake wa kuomba dua.

snura dua (2)Juu ya tetesi kuwa fedha alizotumia kupangia nyumba hiyo zilitokana na malipo aliyopata kwenye kampeni, alikana na kudai zinatokana na udundulizaji wake alioufanya kwa muda mrefu, kwani fedha za kampeni haziwezi kumtosha kwa vile riziki anayopata yeye, hugawanyika sehemu nyingi.

snura dua (1)“Ukiniambia kuwa pesa ya kampeni ndiyo imenifanya nimepanga nyumba hii kubwa utadanganya, kwani pesa ninazopata huwa zinagawanyika sana, zinaenda sehemu nyingi jambo ambalo siwezi kukwambia na hii niliyopata ndiyo haswaaa, ila nilikuwa nikijiwekea akiba kidogokidogo  tangu siku nyingi,” alisema Snura.

Leave A Reply