SOKO LA MASTAA WA KIKE BONGO KUHAMIA DUBAI…SIRI YAFICHUKA!

IMEFICHUKA! Baada ya awali mastaa wengi Bongo kuonekana kukimbilia sana nchini China, Ijumaa Wik­ienda limebaini kuwa kwa sasa mastaa wengi hususan wa kike, soko lao limeha­mia nchini Dubai huku siri kadhaa za wanachokifuata zikitajwa.  

 

Mnyetishaji wetu aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa mastaa wetu mara ny­ingi wamekuwa wakionekana kwenda Dubai ambapo hujia­chia na kuonekana kwenye mitandao lakini nyuma ya pazia kuna siri zinazowape­leka.

“Wengi wao wameanzisha biashara ndogondogo za manukato na udi, vitu hivi vinapatikana kiurahisi huku lakini wengine wana soko kubwa la kisanii ndiyo maana wanakuja huku,” alisema sosi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jamila. Aidha, Jamila alidai kuwa hata hivyo pamoja na wao kufanya biashara lakini wapo wanaofika mjini hapo kwa ajili ya kudanga ambapo hukutana na wanaume wenye fedha zao na kuwawezesha.

“Wapo wanaofika huku kwa ajili ya kudanga wanaume wa Kiarabu wanatoa dau kubwa sana kwa wasanii ndiyo maa­na wakifika huku wanajiachia kwani bata wanalopewa si la nchi hii,” alisema sosi huyo.

Sosi alienda mbali zaidi na kudai kuwa, mbali na hao wanaopenda kwenda ku­danga, watu wa Dubai huwa wanawapenda sana wasanii au watu wenye majina hivyo huwapapatikia na kuwaone­sha ukarimu hivyo ni rahisi mtu kupata rafiki ambaye ana uwezo wa kumgharamia kwa kila kitu.

Wapo wanaokwenda kwa ajili ya kutumbuiza kwenye sherehe za harusi mbalimbali na sherehe za watu binafsi, lakini wapo wanaopiga shoo kama vile mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’. Baadhi ya mastaa waliofika Dubai na kufunguka yaliyow­apeleka ni pamoja na Halima Yahya ‘Davina’ ambaye alisema amekuwa akienda kwa ajili ya biashara yake ya manukato. 

Aunt Ezekiel naye ame­kuwa akienda mara kwa mara Dubai lakini alieleza kuwa mara nyingi huenda kwa ajili ya mapumziko ambapo hivi karibuni alikwenda kushere­hekea siku yake ya kuzaliwa lakini mpaka sasa (juzi) yupo nchini Dubai akiwa na kundi la mastaa wenzake; Jacque­line Wolper, Vivi pamoja na Davina ambapo wanadaiwa kwenda kwenye sherehe ya kibao kata.

Staa mwingine aliyewahi kwenda Dubai ni pamoja na Irene Uwoya ambaye alikwen­da kwa ajili ya mapumziko pamoja na rafiki yake. Mbali na wote Kajala Ma­sanja naye amewahi kwenda Dubai ambapo alikwenda kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Loading...

Toa comment