The House of Favourite Newspapers

Southgate: Ni Bahati Sancho Kuitwa England

0

KOCHA wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amesema ni kama bahati tu kumuona mshambuliaji Jadon Sancho yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England.

Sancho amekuwa hana mafanikio makubwa kwenye timu ya Manchester United ambayo amejiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Borussia Dortmund sehemu ambayo alikuwa akionyesha kiwango cha juu.

Awali ilielezwa kuwa Southgate alitaka kumuondoa winga huyo kwenye kikosi chake lakini akaona kuwa atamchanganya zaidi ndiyo maana akaamua kumuita.

“Tumekuwa na Jadon kwa muda mrefu na tumewekeza sana kwake, tunaamini kuwa anaweza kubadilika huko mbele na kufanya vizuri zaidi.

“Ni kama bahati kumuona kwenye kikosi cha England kwa kuwa hajapata nafasi ya kutosha ya kucheza, lakini kwa kuwa ni kijana wetu hakuna jinsi,” alisema kocha huyo.

MANCHESTER, England

Leave A Reply