The House of Favourite Newspapers

Spika Job Ndugai Awaagiza Polisi Wamkamate Mbunge Halima Mdee

DODOMA: Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempa saa 24 Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee awe amefika bungeni mwenyewe au akamatwe na polisi popote pale alipo kwa tuhuma za kumtukana bungeni.

Mdee anadaiwa kutoa lugha za matusi kwa Spika Ndugai wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika juzi Jumanne, April 4,2017.

Ndugai amesema, “Kama atakaidi amri hiyo basi aletwe katika mamlaka ya Bunge hata akiwa na Pingu”

Comments are closed.