The House of Favourite Newspapers

Vita ya Idadi ya ‘Followers’ Insta na Kiburi cha Watumiaji

“MIMI ni mtu mkubwa, nina wafuasi (followers) wengi sana kwenye mtandao wangu wa  Instagram ‘Insta’, unacheki walivyokuwa wengi, wamefi ka milioni moja sasa.”

Hayo ni maneno ambayo unaweza kuyasikia kutoka kwa mastaa wakijitapa kwamba, wao wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii. Dunia imebadilika, imekuwa kama kijiji, kule ambapo unapaona mbali, kwamba huwezi kupata habari zake, sasa hivi unazipata tena kwa urahisi sana ndani ya muda mchache tu.

Watu wanapigana vita kila kukicha kuhakikisha kwenye Insta zao kukisomeka hivi; POST 223, FOLLOWERS 995,000, FOLLOWING 634, kwamba wafuasi ni wengi sana kuliko mhusika kutuma posti zake au yeye kuwafuata wengine (following), yaani yeye kuwa mfuasi wa watu wengine.

KUJIAMINI HUANZIA HAPO

Tunapongeza mabadiliko japokuwa kwa huku kwetu Tanzania, sehemu ambayo ndiyo yanaendelea kukua tunaona ni vitu vigeni sana kiasi kwamba, unapopata wafuasi wengi kwenye mitandao hiyo mtu anaamini kwamba yeye ndiye unakubalika, yeye ndiye ‘top’ kuliko watu wote na kuanza kuwadharau wale wenye wafuasi wachache.

MTAZAMO HASI Kuna kitu Watanzania ni lazima tuelewe kwamba, kuwa na wafuasi wengi kwenye Insta au hata Facebook, si kukubalika katika jamii. Unaweza ukawa na wafuasi wengi halafu kwenye jamii ukaonekana mtu wa kawaida kuliko yule mwenye wafuasi wachache.

Mitandao imewekwa kwa ajili ya kuwasiliana, imewekwa kwa ajili ya kujitengenezea pesa. Katika mitandao hiyohiyo wengine wamejiona kuwa kila kitu, unaweza kuwa na wafuasi milioni moja (1,000,000), lakini ndani ya watu hao, wanaokukubali ni laki moja (100,000) tu, laki tisa (900,000) wapo wapi? Wanafanya nini?

Haimaanishi ukiwa na watu milioni moja wote watakuwa wafuasi wako, kwamba wote watakuwa wakikupenda, kwamba chochote utakachokifanya, hata kama ni ujinga basi watu wote watakuunga mkono.

Hakuna kitu kama hicho. ANGALIA MFANO HUU Kuna mifano mingi hai. Mwangalie msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Nigeria, Wizkid, ana wafuasi wengi Instagram ambao ni milioni 3.3 kuliko hata Mbongo mwenzetu, Ali Kiba mwenye wafuasi milioni 1.9 lakini cha kushangaza, Ali Kiba alimshinda Wizkid katika Tuzo za MTV mwaka huu ambazo asilimia kubwa, kura zilipigwa katika mitandao.

Hapo utagundua kwamba, kuwa na wafuasi wengi hakumaanishi kwamba unapendwa na kila mtu, haimaanishi kwamba utaheshimika na kila mtu. Mwingine anakuwa mfuasi wako kwa ajili ya kuangalia picha zako, posti zako na vitu vingine lakini akawa hakupendi tu.

MFUASI KUKUTUKANA

Ukitaka kuliamini hili, angalia kwenye posti hizohizo, watu ambao wamemfuata msanii fulani wanaanza kumtukana matusi ya nguoni kwenye Insta! Watanzania inabidi tujifunze, kuna kitu hapa kwamba tusichukulie wafuasi wengi wa mitandaoni ndiyo heshima, inawezekana ukawa na wafuasi milioni moja ila kama ingekuwa wale wanaokukubali ni wangapi, usishangae ukakuta una laki tatu tu.

KUOTA MAPEMBE MITANDAONI KUNATOKA WAPI?

Inamaana watu wamekuwa malimbukeni mpaka kuona kwamba kuwa na wafuasi wengi ni kukubalika? Inamaana mtu anakuwa limbukeni wa mitandao ya kijamii kiasi cha kumwambia mwingine nitakuweka utukanwe? Ulimbukeni huo umeanza lini? Ni elimu ndogo? Uwezo mdogo wa kufi kiri au tuseme ni kutokujitambua?

Wenzetu wa ‘majuu’ (nchi zilizoendelea) wana akili sana, wanajitambua ndiyo maana akaunti zao haziandiki  kuhusu vijembe, wapo radhi kuongea vijembe katika redio na televisheni lakini si kwenye akaunti zao.

Wanajua kwamba, kwenye akaunti kuna maadui zao, si kila aliyekuwa kule ni mwenzao lakini kwetu sisi, kila mtu unayemuona ‘kakufolo’ kwenye akaunti yako ukahisi ni mwenzako, unaota mapembe kwa kudhani kwamba ukiandika utumbo wako, basi wafuasi wako milioni moja wote watakusifia kumbe mwimwisho wa siku unatukanwa na kuonekana HUFAI.

JIKAGUE KWA KUFANYA HIVI

Ukitaka kuamini kama unafuatiliwa na watu wote hao, hebu weka video, halafu angalia ni watu wangapi wameitazama video yako. Wafuasi wako ni wale wanaoingia kwenye akaunti yako kila leo, kama una wafuasi milioni moja halafu umeweka video na kutazamwa na watu elfu thelathini, basi jua wengine wamekuwa wafuasi wako kwa kuwa una jina lakini uposti, usiposti yeye halimuhusu.

Sasa inakuwaje mpaka mtu huyu kumuita shabiki wako namba moja? Huwezi kupendwa na wote na huwezi kuchukiwa na wote. Unapoanzisha kitu kwenye mitandao ya kijamii ni lazima ujue kwamba wewe si lolote lile, hata kama Mungu angeanzisha akaunti yake (ni mfano tu) bado kuna watu wangetukana kwa kumwambia kwamba hawaamini kama yupo (nasisitiza ni mfano tu).

Hata Yesu Kristo na Mtume Muhammad walipingwa na watu, hawakupendwa na kila mtu, sasa iweje wewe ujione staa, kwamba utapendwa na kila mtu? Hakuna mtu kama huyo duniani.

JIFUNZENI HAPA

Wasanii inabidi mjifunze, na si kwa wasanii tu, hata kwa wale watu mlio na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii mjue kwamba si kila mfuasi aliyekufolo ni wako, kwamba anakukubali hata kama utafanya ujinga gani. Unatakiwa kuwa smati, uwe na akili ya kuendana na watu hao.

Unaweza kumbadilisha mtu, akawa amekufolo kikawaida lakini kutokana na posti zako ukamfanya kuwa shabiki wako namba moja. Hilo ndilo linalotakiwa kufanywa, ila ukiandika utumbo kila siku, kuweka picha za utupu, utabaki na wafuasi jina lakini kiukweli hawapo na wewe gani watu hao.

Unaweza kumbadilisha mtu, akawa amekufolo kikawaida lakini kutokana na posti zako ukamfanya kuwa shabiki wako namba moja. Hilo ndilo linalotakiwa kufanywa, ila ukiandika utumbo kila siku, kuweka picha za utupu, utabaki na wafuasi jina lakini kiukweli hawapo na wewe.

 

 

Comments are closed.