The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Jumanne Yaja Kivingine, Wasomaji Kufaidika Mpaka Basi!

0

KAMPUNI ya Global Publishers kupitia gazeti lake bora la michezo la Spoti Xtra, imekuja na Chemsha Bongo kwa wasomaji wa gazeti hilo ambapo washindi watakuwa wakipewa zawadi mbalimbali za vyombo vya ndani ikiwemo friji, brenda, microwave na vingine vingi.

Chemsha Bongo hiyo inakwenda sambamba na ujio wa Gazeti la Spoti Xtra Jumanne ambapo wiki hii ni mara ya pili linaingia mtaani. Awali Spoti Xtra lilikuwa likitoka mara mbili kwa wiki, Alhamisi na Jumapili, lakini sasa litakuwa linatoka mara tatu kwa wiki. JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI kwa bei ileile ya Sh 500.

Akizungumzia Chemsha Bongo hiyo, Mhariri wa Spoti Xtra, Omary Mdose, alisema: “Kwa kushirikiana na Vunja Bei ambao ni wauzaji wa vyombo vya ndani hapa nchini, tumekuja na Chemsha Bongo kwa ajili ya Gazeti la Spoti Xtra ambalo kwa sasa linatoka mara tatu kwa wiki.

“Tunatarajia kutoa zawadi kwa washindi 100 ambapo zawadi zenyewe ni vyombo vya ndani kama friji, brenda, microwave na vinginevyo.”

Leave A Reply