The House of Favourite Newspapers

Stamina Ageukia Uandishi wa Vitabu

0

MSANII anayefanya vyema kunako kiwanda cha Hip Hop nchini Bonivanture Kabonga ‘Stamina’ amefunguka kwamba mbali na kazi za muziki, mwaka huu mashabiki zake wategemee pia kupokea kazi zake za uandishi ambapo ana mpango wa kuachia vitabu pamoja na makala mbalimbali.

 

Msanii huyo ambaye Februari 8, mwaka huu aliachia makala yake aliyoipa jina la Kivuli Cha Ndoa, ambayo inatajwa kueleza kinagaubaga masuala mbalimbali na misukosuko wanayokutana nayo wanandoa, ameonekana kunogewa na uandishi na ameamua kuelekeza nguvu zake katika tasnia hiyo.

 

“Naamini mimi ni mwandishi mzuri, nimeanza na makala ya Kivuli Cha Ndoa ambayo hadi sasa inafanya vizuri sana kwani nimepokea pongezi kwa watu mbalimbali, lakini sitaishia hapo, mwaka huu mbali na kuachia kazi za muziki, lakini pia nimepanga kuingiza sokoni vitabu kadhaa. Pia makala zinazohusiana na mada mbalimbali zitakuja,” alisema Stamina.

Leave A Reply