The House of Favourite Newspapers

Stars Kuondoka Kesho Mechi ya Marudiano na Rwanda

0

TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars, itaondoka kesho saa 4.00 asubuhi mjini Mwanza kwenda mjini Kigali, Rwanda, kwa ajili ya mechi ya marudiano na wenyeji, Amavubi raundi ya kwanza kuwania tiketi ya fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Kenya.
Baada ya sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Jumamosi, Stars na Amavubi zitarudiana Julai 22 Uwanja wa Amahoro, Kigali, katika mchezo wa kuamua timu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda, amesema kwamba yamefanyika mabadiliko na sasa Taifa Stars ya kocha Salum Shaaban Mayanga itaondoka Jumatano badala ya Alhamisi, ili kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji pamoja na hali ya utulivu wakiwa nchini Rwanda kabla ya  mchezo huo.

Na Ester Msofe/GPL

Leave A Reply