The House of Favourite Newspapers

Stars Yatibua Ulaji wa Kocha wa Sudan

ZDRAVKO Logarusic raia wa Crotia ambaye ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Sudan hali ni tete kwenye benchi la ufundi kutokana na kushindwa kutimiza lengo la kwenye mkataba la kuhakikisha anafuzu fainali za Chan.

 

Stars imeongeza ugumu kwa bosi huyo kuitwa mezani tena kutokana na kupindua meza kibabe kwa ushindi wa mabao 2-1 na kufanya idadi ya mabao kuwa 2-2 na Stars kufuzu kwa faida ya bao la ugenini.

 

Logarusic aliyejiunga na Sudan Desemba 2017, mkataba wake umefika ukingoni na inaelezwa kuwa mabosi walikuwa wanamsikilizia afuzu michuano ya Chan ambayo inawahusisha wachezaji wa ndani kwa kuwa amechemsha basi kuna hatihati atapigwa chini mazima.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Logarusic muda mchache kabla ya mchezo alisema kuwa ushindi wake mbele ya Tanzania ulikuwa umeshikilia mkataba wake mpya.

 

“Nimekaa na timu kwa muda mrefu na mkataba wangu kwa sasa upo ukingoni na hakuna dalili zozote ambazo mabosi zangu wamezionyesha hivyo baada ya mchezo dhidi ya Tanzania hatma yangu itajulikana.

 

“Mpango wa kubaki huku sina uhakika kwa kuwa mimi ninaujua uwezo wangu na ninatambua mbinu nyingi, sina mashaka endapo sitaongezewa mkataba ndani ya timu ninayosimamia kwa sasa,” alisema Logarusic ambaye aliwahi kuikochi Simba.

Comments are closed.