The House of Favourite Newspapers

Sugu, Mkewe Wapata Mtoto, Wamwita ‘Freeman’

0

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II Sugu, ametoa taarifa ya kupata mtoto mwingine na mkewe Happiness Msonga.

 

Akitoa taarifa hiyo kupitia post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Joseph Mbilinyi ameandika kuwa.

 

“Taarifa, mimi na familia yangu tunaendelea kumshukuru sana Mungu, asubuhi ya leo ametujalia kupata mtoto mwingine, amezaliwa kwenye Hospitali ya wazazi Meta jijini Mbeya na tumempa jina la Freeman, asanteni.”

 

Kwa sasa Joseph Mbilinyi ana jumla ya watoto watatu ambao ni Shawn na Freeman Joseph Mbilinyi akiwapata kwa mkewe Happiness Msonga, huku mtoto wake wa kwanza Sasha alimpata alipokuwa na mfanyabiashara Faiza Ally.

Leave A Reply