The House of Favourite Newspapers

Sven Ataja Sababu Ya Kumtema Mugalu

0

BAADA ya Simba kuwaacha nyota wake watatu Chris Mugalu, Charles Ilanfya na David Kameta uongozi wa timu hiyo umefunguka juu ya sababu za kuwaacha nyota hao.

 

Simba jana Jumanne walisafiri kuelekea nchini Nigeria tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau FC ya nchini huko, mchezo ukitarajiwa kufanyika wikiendi hii.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck alisema kuwa majeruhi ya Mugalu na kutokuwa fiti kwa Ilanfya ni sababu ya kuwaacha nyota hao huku Kameta yeye akiachwa kutokana na kuwa katika majukumu ya timu ya taifa chini ya umri wa miaka 20, ambao wapo katika michuano ya CECAFA inayoendelea kufanyika mkoani Arusha.

 

“Wachezaji ambao wameachwa wote wana sababu zao mbalimbali na ukiziangalia ni za msingi katika mpira wa miguu na ndiyo maana umeona kuwa tumewaacha na si mambo mengine kama watu wengi ambavyo wanafikiria.

 

“Mugalu bado ni majeruhi na kwa Ilanfya yeye bado hayupo fiti hivyo hayupo tayari kwa mchezo huu na kuhusu Kameta yeye yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, hivyo pia tusingeweza kuwa naye katika safari yetu,” alisema kocha huyo.

 

Mugalu ambaye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu tayari ana mabao matatu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na anatajwa kuwa kati ya washambuliaji mahiri zaidi lakini akiwa anasumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply