The House of Favourite Newspapers

Tabasamu la DC Jokate baada ya Kukutana na Wadau Hawa


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amepokea msaada wa Taulo za kike kutoka kwa Kikundi cha Wakunyumba ambacho kimemsapoti kwa lengo la kuunga mkono juhudi zake hasa za Tokomeza Zero Wilaya ya Kisarawe.

Baadhi ya viongozi wa Kikundi cha Wakunyumba wakimkabidhi msaada wao.
Picha ya pamoja na DC Jokate.

 

KIKUNDI cha Wakunyumba Group kilianzishwa 17/11/2018 kikitokana na group la WhatsApp la vijana wa mkoa wa Luvuma ambao wanaishi jijijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wakikabidhi msaada huo Meneja Mratibu wa kikundi hicho, Robert Nchimbi alisema kuwa kikundi chao kilianza wanachama saba lakini hadi sasa kina wanachama 31.

 

Alisema kuwa lengo kubwa la kikundi hicho ni kuhakikisha kinawasaidia wao kwa wao katika shida mbalimbali na kusaidia jamii yenye kuwa na uhitaji maalum.

Aidha alisema kuwa lengo lingine la kikundi hicho ni kuhitaji kuanzisha mradi wa ushonaji ambao utawezesha uzalishaji wa ajira kwa watanzania nchini kupitia ushonaji nguo.

 

Comments are closed.