UKIANGALIA kwenye viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), utaikuta Tanzania ipo nafasi ya 125. Nafasi hiyo si nzuri kwani inadhihirisha kwamba tumeshuka sana na hatuna uwezo wa kupambana na vigogo.
Nakumbuka nafasi hiyo ya 125, tuliipata mwezi Agosti ikiwa ni miezi miwili imepita tangu tushike nafasi ya 116. Ukiangalia hapo ndani ya miezi mitatu tumeshuka kwa nafasi tisa.
Si jambo la kufurahisha kuona kila kukicha tunaporomoka kwenye viwango vya Fifa, kinachotakiwa ni kuiandaa vizuri timu yetu ili iweze kutoa ushindani na kushinda katika michezo mbalimbali ya kirafiki na kimashindano ili ipande juu. Tutoke huku tulipo sasa.
Katika kuiandaa vizuri timu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lina jukumu la kuhakikisha kila kwenye Kalenda ya Fifa tucheze mechi ambazo ndizo zitatupandisha kule tunapopataka.
Kucheza mechi nyingi inawajengea kujiamini w a c h e z a j i ambapo hata kama ikitokea tumefungwa, basi naamini siku zijazo baada ya kujiamini wa t a t u l e t e a matokeo mazuri. Tutakuwa tumetatua tatizo lililopo.
Kusema TFF ina jukumu la kutafuta mechi za kirafiki kwa Taifa Stars s i m a a n i s h i kwamba hivi sasa hawatafuti, bali ni kuendelea kufanya hivi inavyofanya sasa.
Nafahamu leo Jumamosi, Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kirafiki uliopo kwenye Kalenda ya Fifa dhidi ya Malawi. Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni muhimu kwetu kwa sababu matokeo ya ushindi yata t u f a n y a tuwe na nafasi nzuri ya k u p a n d a katika viwango vya Fifa jambo a m b a l o tumekuwa tukilihitaji kwa muda mrefu.
M b a l i n a kupanda k w e n y e viwango h i v y o , lakini pia itatusaidia katika maandalizi yetu ya mechi za kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kwa mwaka 2019.
Tukitumia vizuri michezo hii ya kirafiki, itatupa matokeo mazuri si leo, bali hapo baadaye kwa sababu bado kikosi chetu kipo kwenye hatua za kujengwa na kweli kinajengeka.
Nikiitazama Taifa Stars ya sasa, naiona bado ipo kwenye maandalizi makubwa ambayo siku zijazo kama ikiwa na mwendelezo huu basi itatufikisha mbali.
Tangu Kocha Salum Mayanga akabidhiwe kikosi hicho, amekuwa akijitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha anakuwa na vijana wengi ambao wataisaidia timu hiyo kufanya vizuri.
Mayanga amekuwa na juhudi kubwa ya kuwatafuta wachezaji wa Kitanzania wanaocheza soka nje ya Tanzania ambao siku za nyuma hawakuwahi kuitumikia Taifa Stars.
Anachokifanya Mayanga kinatakiwa kuwa na mwendelezo hata kama ikitokea siku ameondolewa kwenye nafasi hiyo kwa sababu tunafahamu licha ya kuaminika, lakini hatoweza kudumu milele.
Bado naamini kuna Watanzania wengi wapo nje ya nchi hii wanacheza soka na kama wakiitwa basi watakuwa na msaada mkubwa kwa taifa letu.
Huku tukiwa tunaipambania Taifa Stars, tusizisahau timu zetu nyingine za taifa, kuanzia ile ya chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys ambayo mwaka 2019 itashiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa umri huo itakayofanyika hapa Tanzania. Pia tusiisahau U-20 na U-23 pamoja na zile za wanawake.
Wikiendi iliyopita tu, timu yetu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite, ilifungwa mabao 6-0 ikiwa nyumbani katika mchezo wa kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya wenzao wa Nigeria maarufu kama Falconets.
Kipigo hicho kinaenda sambamba na kile cha mabao 3-0 ambacho walikipata ugenini na kuwafanya kuondoshwa kwa jumla ya mabao 9-0.
Tukiwekeza katika timu zetu zote za taifa, naamini tutapiga hatua kuanzia soka la wasichana mpaka la wavulana.