The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars Yaitwanga Botswana 2-0

0
Mbwana Samatta akiambaa na mpira.

TIMU ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imeinyuka Timu ya Botswana bao 2-0, mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA ambao umepigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Taifa Stars.

Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa Stars, Simon Msuva anayekipiga Difaa Eljadida ya Morocco ameibeba Tanzania baada kupachika bao zote mbili ambapo bao la kwanza amefunga dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza na kurudi tena wavuni kunako dakika ya 61 ya mchezo huo.

Stars wakishangilia bao la kwanza la Msuva.

Kunako dakika ya 20, Mbwana Samatta alimchomekea Msuva pasi maridadi ambayo alizama nayo moja kwa moja langoni kwa kuachia mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Botswana na kuwafanya Watanzania kunyanyua vinywa wakishangilia bao hilo.

Msuva akiwatoka mabeki wa Botswana.

Mchezo ulikuwa mzuri na wa kusisimua huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu licha Stars kuwazidi mbinu Botswana na kuibuka na ushindi huo.

Stars wakishangilia bao.

 

Himid Mao akiachia shuti kali.

 

Samatta akifanya yake.

 

 

Msuva akijaribu kuwatoka mabeki wa Botswana.

 

Msuva akitibiwa baada ya kuumia.

 

Kikosi cha Botswana.

 

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

SHUHUDIA Msuva Alivyong’ara Baada ya Kupachika Mabao 2-0

Leave A Reply