The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (17)

0

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (17)

 

ILIPOISHIA…

Nadhani hata yeye pamoja na kutisha kwake na uajabuajabu aliokuwa nao, alishangaa kwa jinsi nilivyosimama kwa ujasiri. Alipofika akasimama na kutimua vumbi jingi. Nikamtazama usoni, uso wake ulitanda giza, lakini nilipoendelea kumtazama zaidi, sura yake ikaonekana. Sura ilipakwa unga mweupe usoni, meno ya pembeni yalikuwa marefu na alipopanua kinywa chake kilitisha kwa jinsi kilivyokuwa kipana.

 

ENDELEA KUISOMA…

Kama nilivyomtazama, naye alinitazama. Macho yake hayakuwa ya kawaida. Isingekuwa kukata tamaa na maisha ni lazima ningekimbia. Lakini niliamua kupumzika na purukushani za walimwengu. Nilisimama.

 

Nadhani alipenda sana kunikimbiza. Alipoona sikimbii, akaaanza kunitisha ili nikimbie apate raha yake ya kunifata mbiombio. Kwanza alitoa sauti za kutisha. Niliogopa lakini sikukimbia. Pili, aliunyanyua upanga wake wenye makali kuwili akawa anatisha kunikata. Niliogopa nikafunga macho ili upanga utue taratibu. Lakini hakunidhuru. Moyoni nikajipongeza kwa kuchukua maamuzi haya madhubuti.

 

Alifanya vimbwanga vingi nikabaki nimesimama nisiyekimbia kama alivyopenda. Naye kuona hivyo hakukubali kushindwa, akajibadili na kuwa chatu mkubwa. Loooh! Sikusimama, nilikimbia bila kukumbuka ule msimamo niliojiwekea. Nilichomoka kama punda wa Bruda. Nikakata kona ya Msamariamwema, kisha nikakunja barabara ya Mwendapole, nikanyooka katika viunga vya Mchopezo kisha vichochoro vya Hujuma, na bila kujitambua nilikuwa chumbani kwangu, nimejifunika shuka zito gubigubi, naogopa kila kitu, hata mapigo ya moyo yalipodunda nilishtuka nikidhani ni zile tambo za kukimbizwa na yule mnyama mbaya!… BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Leave A Reply