The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars yajipa kazi ya kushinda Kenya

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana Jumapili ilishindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Kenya katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (Chan).

 

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulishuhudiwa na mashabiki wachache waliojitokeza uwanjani hapo.

 

Stars ililisakama lango la Kenya kwa muda mrefu na kipindi cha kwanza kilimalizika wakiwa wanaongoza umiliki kwa 60/40 lakini hawakuweza kuwa na makali ya kufunga bao. Stars ilipata nafasi tatu za wazi katika kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuzitumia vizuri kupata bao.

 

Kipindi cha pili, Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ayoub Lyanga na kumuingiza Ibrahim Ajibu dakika ya 54, pia walimtoa Hassan Dilunga wakamuingiza Kelvin John dakika ya 66 lakini hawakuweza kubadili kitu. Dakika ya 84 Stars walifanya mabadiliko tena kwa kumtoa John Bocco na kumuingiza Salim Aiyee lakini bado hawakuweza kuipenya ngome ya wapinzani.

 

Sasa Taifa Stars itatakiwa kushinda au kupata sare ya mabao dhidi ya Kenya katika mchezo wa marudiano Jumapili ijayo ili iingie kutinga katika hatua nyingine ya mtoano.

 

Kikosi cha Stars kilichoanza ni Juma Kaseja, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Hassan Dilunga, John Bocco, Ayoub Lyanga, Paul Godfrey ‘Boxer’, Jonas Mkude na Idd Selemani ‘Nado’. Kenya: John Oyemba, Bernad Oginga, Clifton Miheso, Joash Achieng, Mike Evans, Dennis Odhiambo, Musa Wanyama, Whayvone Kinyangi, Enosh Ochieng, Kenneth Mugambi na Duke Ooga.

HABARI: IBRAHIM MUSSA, GPL

Comments are closed.