The House of Favourite Newspapers

Tajiri Aendelea Kusaka Namba Ya Wema

0

BAADA ya habari za Wema Sepetu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hana gari, yupo tajiri mmoja mwenye maskani yake nchini Marekani ambaye ameendelea kusaka namba ya simu ya mwigizaji Wema Sepetu.

Tajiri huyo amekuwa akitangaza mitandaoni kwamba, alikerwa mno na na kauli ya Aristostle kwamba Wema hana gari kama mastaa wengine akipambanishwa na mwigizaji mwenzake, Irene Uwoya.

“Nimeamua kusaka namba ya Wema kwa sababu vitu ambavyo Aristostle alivusema kwa Wema vimeniumiza, naomba tuheshimu wamama, kila mwanamke ni mama yako, Aristotle heshimu wamama, sasa nimeamua, nataka nimpatie pesa Wema Sepetu ili naye anunue gari la kifahari,” anasema jamaa huyo.

Kwenye video ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, inaonesha tajiri huyo akiwa anaonesha begi liliojazwa pesa huku akieleza anataka kumkabidhi Wema pesa hizo ili anunue gari.

“Hizi ni Dola 100,000 kwa pesa za Kitanzania ni shilingi million 250, nampa Wema anunue gari, mwenye namba yake anitumie kwa DM,” anasema jamaa huyo.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply