The House of Favourite Newspapers

TAKUKURU Yaanza Kumshughulikia Kangi Lugola

0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (Takukuru) leo inatarajia kuanza kuwahoji viongozi mbalimbali waliohusika na mkataba wa zaidi ya Tsh trilioni 1, akiwemo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, JOHN MBUNGO amesema walianza kukusanya taarifa za awali ambazo zimeshakamilika na wahusika wote wataitwa kesho kuhojiwa.

 

Wengine watakaohojiwa ni aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andegenye; Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.

 

Pia wapo naibu katibu mkuu wa wizara hiyo, Ramadhan Kailima; watumishi wa wizara hiyo na wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania. Wanahojiwa kutokana na mkataba kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kampuni moja ya Romania kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali vya jeshi hilo.

 

Januari 23, 2020 Rais wa Tanzania, John Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa Lugola na Andengenye huku akiridhia barua ya kujizulu ya Meja Jenerali Kingu na kuagiza Takukuru kuanza uchunguzi kwa wote waliohusika bila kujali nafasi zao. Tayari Rais Magufuli amemteua Kingu kuwa Balozi na anasubiri kupangiwa kituo cha kazi.

 

Juzi Alhamisi, Januari 29, 2020, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo na kusema, “Wameanza kufanyia kazi maagizo ya Rais kwa kukusanya nyaraka na Ijumaa (kesho) tutakutana na Lugola katika ofisi za jijini Dodoma.”

 

Leave A Reply