The House of Favourite Newspapers

Tanasha: Kulea Mwenyewe ni Presha Kubwa!

0

“Siyo kazi rahisi kulea mwenyewe, presha ni kubwa mno, lakini ninakabiliana nayo…”Hayo ni maneno ya mwanamama Tanasha Donna alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini kwao, Kenya juu ya malezi ya mtoto Naseeb Junior aliyezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Tanasha ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, anasema kuwa, anafanya kazi kwa bidii mno kuhakikisha anampatia mwanaye kila kinachohitaji, lakini kamwe siyo jambo rahisi kufanywa na mtu mmoja.

 

Mama huyo wa mtoto mmoja wa kiume anasema kuwa, amekuwa akipitia kwenye presha kubwa na inamlazimu kutokwa jasho la kutosha ili kumtimizia mwanaye huyo mahitaji stahiki.

Hata hivyo, Tanasha anaendelea kusema kuwa, atahakikisha Naseeb Junior hakosi kwa kuwa Mungu yupo upande wake.“Kamwe haijawahi kuwa kazi rahisi kwa mtu mmoja kulea mwenyewe, ni presha kubwa, lakini ninapambana nayo…”

 

Anasema Tanasha ambaye alitengana na Diamond au Mondi mapema mwanzoni mwa mwaka huu huku akilalama kutelekezwa na jamaa huyo kwenye suala zima la malezi ya mtoto wao huyo

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, IJUMAA

Leave A Reply