The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Kipa wa Kagera Sugar Afariki Dunia, Bugando Hospital

david-buruhan-kagera-sugar-1

TASNIA ya mchezo wa soka hapa nchini imekumbwa na majonzi makubwa, baada ya  mlinda mlango wa Klabu ya Kagera Sugar na mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa PAN, Abdallah Buruhan, David Buruhan kufariki dunia leo katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

david-buruhan-kagera-sugar-2

Taarifa za awali za msiba huo zimeelezewa kuwa, David aliugua ghafla wakati wakiwa njiani na klabu yake kuelekea mkoani Singida kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam, waliporudi Kagera hali yakeilibadilika na kuwa mbaya ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Bugando kwa ajili ya mayibabu ambako umauti umemkuta.

david-buruhan-kagera-sugar-3

Mwenyekiti wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein pamoja na rafiki wa marehemu Paul Nonga wa Mwadui Fc wamethibitisha kutokea kwa msiba huo.

Hakika hili ni pigo kubwa kwa wakazi wa Kagera, Klabu ya Kagera Sugar na familia ya soka hapa nchini.

Daima tutakukumbuka David Buruhan!

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu David pema peponi!

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.