The House of Favourite Newspapers

TANZIA: Mama Vicky Nsilo Swai Afariki Dunia

0

Mama Vicky Nsilo Swai aliyekuwa mke wa mwanasiasa mkongwe, mpigania uhuru na waziri wa zamani, Asanterabi Nsilo Swai, amefariki dunia, taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi.

 

Enzi za uhai wake, Mama Swai aliwahi kuhifadhi nyumbani kwake viatu vya mpigania uhuru na rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina!

 

Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

 

Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia) Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerzani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.

 

Rais Kikwete akimtambulisha Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere kwa waombolezaji wakati wa shughuli ya mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu Afrika kusini Desemba 15, 2015.

Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu.

Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995

Leave A Reply