Tanzia: Mwanamuziki Tina Turner Afariki Dunia Nchini Uswisi
Nyota huyo mkongwe wa Muziki wa Rock ‘n’ Roll, Tina Turner amefariki nyumbani kwake huko Kusnacht Nchini Uswisi akiwa na umri wa miaka 83 baada ya kuugua kwa muda mrefu
Kwa mujibu wa familia, Turner aliyezaliwa Tennessee, Marekani alianza kuwa na hali mbaya ya Kiafya baada ya kugundulika kuwa na Saratani ya Utumbo mwaka 2016 na kupandikizwa Figo mwaka 2017
Enzi za uhai wake, alifanikiwa kushawishi Wanawake wenye Asili ya Afrika kufanya muziki wa Rock ‘n’ Roll huku akitamba na nyimbo kama ‘Whats Love Got To Do With It’ na ‘Proud Mary’