Tanzia: Mwandishi wa Habari Vedasto Msungu Afariki Dunia

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa ITV na Radio One Stereo aliyebobea katika habari za Mazingira, Vedasto Msungu amefariki dunia leo saa 11 jioni Jumatano Februari 17,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro, Nickson Mkilanya amethibitisha taarifa za kifo cha Vedasto Msungu na kueleza kuwa taarifa kuhusu msiba huo zitaendelea kutolewa.

Toa comment