The House of Favourite Newspapers

Viongozi TZ na Mataifa Wamlilia Maalim Seif

0

 

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali nchini Tanzania na nje ya Tanzania wameomboleza kwa huzuni kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif hamad ambaye amefadunia leo Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 

 

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina,” Rais Magufuli.

 

“Nimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad natoa pole kwa familia na watanzania wote.”  Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

 

Pumzika kwa Amani Mzee wetu, Mh Maalim Seif -Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Familia, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Watanzania wenzangu wote. Pumzika kwa Amani.”  Mwigulu Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria.

 

“Naomba kuchukua nafasi hii kuwafahamisha Watanzania kwamba @SeifSharifHamad alitulea kiuongozi kwa namna ambayo tutaweza kuendeleza maono yake, fikra na nia yake ya kuiona TZ yenye demokrasia na Zanzibar ambayo Wazanzibar wanaishi kwa maridhiano, Zitto Kabwe.

 

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Chama chaACT wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar @SeifSharifHamad. Hili ni pigo kuondokewa na Kiongozi shupavu na mwanamageuzi, Tanzania na Afrika. Tunatoa pole kwa familia, chama chake na Wazanzibari,CHADEMA.

 

“Pumzika kwa amani Maalim Seif. Hakika taifa limepoteza kiongozi shupavu, mahiri na muhimu katika kuwaunganisha wazanzibari! Pole kwa familia, Rais wa Zanzibar na ACT Wazalendo,Waziri Ummy Mwalimu.

 

Hakika ni pigo kubwa sana kwa Taifa letu, ni huzuni na simanzi kwa Watanzania wote, tumempoteza kiongozi imara na icon ya Taifa. Pumzika mzee wetu Maalim Seif Sharif Hamad.” Eric Shigongo.

 

“Pole nyingi kwa Rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi, familia ya marhum na wazanzibari wote kwa msiba huu mkubwa. Inna Lillah Wainna Ilayhi Raajiuun,” Ally Hapi.

 

5 POINTS ABOUT MZEE SEIF SHARIF HAMAD….

1. Amekuwa jabari la kisiasa na mmoja wa wanasiasa nguli barani Afrika na Duniani katika karne ya sasa.

2. Amekuwa Chuo Kikuu cha Kisiasa, yaani he was a Political University by himself, ungeliweza kufanya tafiti nyingi kuhusu siasa zake na fikra zake na ukaandika maelfu ya vitabu na bado ukahitaji kuandika tena na tena.

 

3. He was an institution by himself (alikuwa taasisi inayojitegemea). Alikuwa na uwezo wa kufanya siasa ziwe na mwelekeo fulani na zikatii na mkabaki mnashangaa amewezaje. Kwa sasa siasa za upinzani za Zanzibar hazina tena “mtu taasisi”…hakuna ambaye anaweza kuwa hivyo isipokuwa Seif ambaye sasa hayupo.

 

4. Alikuwa bingwa wa maridhiano na kutaka watu wakae pamoja. Kwenye hili unaweza kumpa digrii 10. Hata kama ungalimuudhi na kumuumiza Maalim kiasi gani, kesho asubuhi angalikupigia simu na kukusalimu na kukwambia bado anakuthamini. Alikuwa na roho ya ajabu sana.

 

5. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusikiliza. Kwenye vikao, ninyi mnaweza kuzungumza masaa 10 yeye anasikiliza na hawezi kuwaingilia, alikuwa anasikiliza sanaaaa. Wakati mnazungumza yeye huandika kila kitu, na haachi hata nukta, halafu yeye anaongea mwishoni kidogo. Muhtasari wake mfupi wa mwishoni ungeliwafanya mjue mwelekeo na mjue nani alibwabwaja na nani alizungumza mambo ya msingi.

 

Narudia, A VERY BIG LOSS TO THE NATION.

R.I.P Mzee.

Your Long Time Political Child, Julius S. Mtatiro.

 

“Nimepokea kwa masikitiko sana taarifa za kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dr. Mwinyi, familia, Wazanzibari, wanachama wa chama cha ACT – Wazalendo na Watanzania wote. Inalillahi wa inailaihi rajeoon 🙏🏽 Mo Dewji.

 

Inna lillah wainna ilayhir rajiuun. This is a tough one. Nimesikitishwa sana na kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. He was a great man. I celebrate his life Kwa sababu kuna somo kubwa kwenye maisha yake; ya kwake Kwa hakika ni maisha ya mpiganaji asiyekata tamaa na aliyekomaa na ndoto yake maisha yake yote.

Natuma salamu za pole kwa ndugu yangu Mhe. Dr. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa Mhe. @zittokabwe, Kiongozi Wa Chama Cha ACT-Wazalendo, wazanzibar wote na wana ACT-Wazalendo wote; Aidha ndugu, jamaa na marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mzito. Apumzike kwa amani Maalim.” Hamisi Kigwangalla.

 

Natoa salamu za pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi kwa msiba mzito wa Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.” Suleimani Jafo.

 

“Zanzibari national independence was Maalim Seif’s raison d’etre. He never wavered in that quest. Years of detention, treason trial, torture and untold hardships didn’t break him. Thru highest highs and bottomless lows, he held high the banner of Zanzibari national aspirations.

 

“My deepest condolences to the family, ACT-Wazalendo, the Zanzibari nation and Tanzanians on the sad passing of Maalim Seif Shariff Hamad. Maalim Seif was the most influential leader and fearless defender of the Zanzibari people and their national aspirations. May he Rest In Peace.” Tundu Lissu. 

 

 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa rambirambi kwa Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein kufuatia kifo cha Makamu wake wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad. Ikulu ya Kenya imeandika katika ukurasa wa twitter alikuwa kiongozi maarufu, mwenye busara na maendeleo na mchango wake kwa watu wake na ukanda wa Afrika Mashariki utakumbukwa.

 

 

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald J. Wright amesema ni kiongozi aliwaweka watu wake mbele kwanza kabla ya madaraka.

Leave A Reply